Shirika Letu

SHIRIKA LA WABENEDIKTINI Wamisionari la St. Ottilien ni mjumuiko wa nyumba za kitawa za Kibenediktini zilizotanda katika mabara manne na nchi 20 kote duniani, likiwa na jumla ya wanashirika 1020 hivi. Watawa hawa wanaishi kadiri ya kauli mbiu ya Kibenediktini ya "Sala na Kazi" (Ora et Labora). Wanashirika hujihusisha pia na shughuli za kichungaji, uendeshaji wa mashule na nyumba za mafungo, mahospitali n.k. Hapa Tanzania Ubenediktini ulikua na kushika mizizi maeneo ya Ndanda, Peramiho, Hanga na Mvimwa. Rais wa Shirika kwa sasa ni Abate Jeremias Schröder akisaidiwa na Bradha Ansgar Stüfe (Mhasibu - Ujerumani). Kati ya Oktoba 2012 hadi sasa kumekuwa na makatibu wa Shrika watatu. Aliyepo sasa hivi ni wa muda (Pd. Maurus Runge wa Königsmünster). Tunategemea kuwa na katika wa shirika wa kudumu hapo Januari 2018. Zaidi >>

Kanda ya Ulaya

Monasteri za Ulaya kwa pamoja zina jumla ya asilimia 37 ya watawa wa Shirika letu. Miaka ya nyuma watawa wengi walipatikana katika monasteri hizo kinyume cha nyakati hizi. Katika Ulaya magharibi tunazo abasia sita, yaani St. Ottilien, Münsterschwarzach, Schweiklberg, Königsmünster, Fiecht na Uznach.

Priorati Tegemezi

Shirika letu limegawanyika kati ya nyumba zinazojitegema na zile ambazo hazijajitegemea bado. Nyumba za aina hii zipo ama chini ya Halmashauri ya Shirika au chini ya nyumba ilizozianzisha. Nyumba tegemezi katika shirika letu ni zile za Tororo Uganda, Kumily India na Havana Kuba. Nyumba zote hizi tatu zipo moja kwa moja chini ya Halmashauri ya Shirika.

Kanda ya Amerika

Wabenediktini Wamisionari walifungua nyumba yao ya kwanza huko Marekani katika jimbo la New Jersey mwaka 1924. Vituo vingine viliendelea kufunguliwa huko Kolombia na Venezuela. Kanda hii inajumuisha El Rosal, Guigwe (Güigüe), Newton, Schuyler na Havana (Kuba).