Kituo cha Zakeo

The gardens...

Baadhi ya Wageni wetu wanakitambua KITUO CHA KIROHO ZAKEO (Spiritual Centre)  kama

P A R A D I S I    Y A    N D A N D A

... na kweli ndivyo Zakeo iliyo. Kituo hiki kimeanza shughuli zake mwaka 2010.  Lengo mama la kituo limekuwa siku zote: Kutoa fursa kwa watu wote: kutulia na kujifunza mambo mbalimbali juu ya imani yao na jinsi ya kuboresha maisha yao kiroho, kimwili na kiakili. Kwa sababu hiyo tunatoa fursa ya kufanya semina za kiroho, nafasi za mikutano, mafundisho ya moyo (ritriti) na warsha mbalimbali. Kama kituo cha Kiroho, Zakeo Spiritual Centre si kituo cha kibiashara. Ni moja kati ya huduma za kitume zinatolewa na Watawa wa Abasia ya Ndanda.

... provide quite environement..

 

... for events...

Huduma Zetu:

o  Nafasi ya Mafungo, Semina na Mikutano kwa Mapadre na Watawa,

o Semina/Mkutano kwa ajili ya Viongozi wa halmashauri za parokia, WAWATA, VIWAWA, LEGIO, TYCS na vyama vinginevyo vya kitume.

o Semina zinazolenga Kuimarisha umoja na mshikamano wa Wana-ndoa (UFATA)

o Semina zinazolenga kuwajengea watu uwezo na weledi katika kunyanyua hali zao za maisha. Kwa kushirikiana na taasisi zisizo ya kiserikali kama vile Agha Khan Foundation, tunatoa nafasi ya kujielemisha katika mambo ya Ujasiriamali.

o Ni lengo la kituo chetu pia kuwa kitivo cha kukuza na kuendeleza maelewano, undugu na ujirani mwema kati ya "WAANA WAWILI WA ABRAHAMU" - yaani Wakristu na ndugu zetu Waislamu.

 

... getting together...etc...

  Kwa vile mwanzoni kituo kilitumia majengo ya jimbo, Askofu G. Mmole wa Jimbo la Mtwara aliiomba Abasia kujenga majengo yake yenyewe kwa ajili ya kituo cha kiroho. Kiujumla ilichukua miaka 14 hadi pale Abasia ilipoweza kuwa tayari kutimiza ombi hilo. Wakati wa maandalizi ya jubilee ya miaka 100 ya uwepo wa Wabenediktini Ndanda mwaka 2006, uamuzi wa kujenga kituo kipya ulifanywa. Kazi ya ujenzi ilianza siku tisa baada ya kilele cha jubilei hiyo hapo 24 Agosti 2006. Mpaka kukamilisha ujenzi wa majengo kwa ujumla ilichukua miaka mitatu na nusu. Mwezi Januari mwaka 2010, Padre Severin alihamia kwenye kituo kipya na kuanza kazi moja kwa moja.  
 

Majengo mapya yana vyumba 21 vya kulala vyenye vitanda viwili kila kimoja na vyumba 12 kati ya hivyo vina vyoo/bafu (self-contained). Eneo lina utulivu wa kutosha, kuna hewa nzuri katika vyumba vya kulala na kuna uwezekano mzuri zaidi wa kufanya mazoezi ya kiroho. Ndani ya Jengo kuna kikanisa kizuri na chumba kwa ajili ya tafakari. Nje vipo vibanda 8 kwa ajili ya kutafakari Biblia na njia inayoongoza kwenye msalaba juu ya kilima.

 
 
 

Siku hizi kituo cha kiroho cha Zakeo kinapata wageni wengi kuliko awali. Majengo mapya na utulivu uliopo ni sababu zinazokipatia kituo sifa na kukubalika na walio wengi. Wageni wanaotembelea kituo hiki wanagundua kuwa sehemu hii inafaa siyo tu kwa ajili ya sala na tafakari ila pia kwa ajili ya mikutano mingine. Kwa wale wote wapendao kufanyia mafungo, semina au warsha katika kituo hiki wanakaribishwa muda wowote kuwalisilana na Mkurugenzi wa Kituo.

<<Mwanzoni