Hospitali

HOSPITALI YA NDANDA

SAMBAMBA na lengo la msingi la kuhubiri Habari Njema, lengo jingine la Wamisionari wetu wa Kibenediktini lilikuwa ni kuhudumia wagonjwa. Utume huu waliufanya tangu mwanzo kabisa wa kazi yao ya kimisionari.

Kushoto: Wodi ya wenye shida za mifupa wakisubiri kupona;

Kulia: Akina Mama vijana wanafurahia baraka ya kupata watoto katika wodi ya akina Mama.

 

Kwa kufanya hivyo waliamini kuwa ujumbe wa upendo wa Kristu ungewafikia watu wote bila kujali tofauti za imani zao. Huduma kwa wagonjwa ilifanywa na masista wamisionari wa Tutzing. Huduma hii ilianzia mnamo mwaka 1900.

Kushoto: Madaktari wapasuaji wakimshughulikia mgonjwa katika Chumba cha Upasuaji cha Hospitali;

Kulia: Daktari wa Meno akimhudumia mgonjwa katika idara ya Meno ya Hospitali.

 
 

Huduma za awali zilielekezwa kwa wagonjwa wa malaria, waathiriwa wa sumu za nyoka, ukoma, n.k. Baada ya Vita Vikuu ya Pili ya Dunia Ndanda iliendelea kukua na hatimaye kuwa hospitali muhimu katika eneo lote la kusini mashariki mwa Tanzania. Hii ilitokana na mchango mkuwa uliotolewa na Sr. Theckla Sinnesbek.

 Kushoto: Akina Mama na Vichanga vyao nje ya Chumba cha Huduma ya Mama na Mtoto;

Kulia: Bwana mdogo Baraka akishangaa atapona lini mguu wake baada ya kuanguka mtini na kuvunjika mguu.

 
 
 

Kwa ushirikiano kati ya Abasia na masista wa Tutzing, hospitali ya Ndanda iliendelea kukua, kuimarika na kutoa huduma za uhakika zaidi kwa wagonjwa. Kwa sasa ina vitanda vya kulaza wagonjwa 300, jengo la kisasa kwa ajili ya upasuaji, idara ya meno, idara ya macho, idara ya mama na mtoto, famasia, chuo cha uuguzi, n.k.


Kushoto: Chumba kimojawapo cha Upasuaji;

Kulia: Daktari Kiongzi wa kitengo cha Upasuaji akionesha baadhi ya mitambo itumikayo katika idara yake.

 
 

Huduma bora zinazolewa na hospitali ya Ndanda zinatambuliwa popote. Kwa sababu hiyo serikali kwa kupitia Wizara ya afya imeipandisha hadhi hospitali yetu kuwa Hospitali ya Rufaa (Consultant Hospital) kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.


Kushoto: Wauguzi wanamchunguza mtoto mchanga baada ya kuzaliwa;

Kulia: Wodi mojawapo ya Wagonjwa. Ili kuepuka malaria matumizi ya neti ni jambo la lazima.

 

<<Mwanzo