Uchungaji

SAMBAMBA NA KUISHI  wito wao wa kimonaki, Wamisionari wa Kibenediktini waliazimia tangu awali kupandiza mbegu ya Ukristo na kuruhusu Kanisa mahalia lichupue, kukua na kujitegemea.  Hata siku hizi parokia mbalimbali zinaongozwa na Watawa wa Ndanda katia majimbo ya Lindi, Mtwara na Tanga.

Parokia ya Ndanda

Baadya ya kituo cha misioni cha Ndanda kuanzishwa mwaka 1906 kiliendelea kukua kwa kasi na umuhimu wake uliendelea kuwa mkubwa Ndanda ilipokuwa makao makuu ya ya Abate/Askofu wa Abasia Nulius ya Ndanda.  Hata baada ya makao hayo kuhamia jimboni Mtwara, Ndanda inabakia bado kuwa kituo muhimu cha kichungaji jimboni Mtwara. Parokia hii ina kiasi cha Wakristu 10,000 katika vigango vya Liputu, Mwena na Mkalapa.

Anuani

Parokia ya Ndanda, SLP Ndanda 

Via Mtwara Tanzania

 

 
 

Parokia ya Nyangao

Kituo cha misioni cha Nyangao kilianzishwa  na Pd. Antonius na Bruda Meinrad mwaka 1896 - kikiwa cha pili baada ya Lukuledi. Nyangao iliendelea kukua na kuwa kituo muhimu cha misioni kwa Wabenediktini wa Ndanda hadi siku hizi. Padri mmoja wa Ndanda anasaidiana na padre wa Jimbo (Lindi) kuongoza parokia hii.

Anuani:

Parokia ya Nyangao.

SLP 1002 Lindi

 
 

Parokia ya Chikundi

Parokia hii ambayo inapatikana katika jimbo la Mtwara iko takriban kilometa 6 magharibi ya Ndanda. Tangu kuanzishwa kwake imekuwa daima chini ya Watawa wa Abasia. Pamoja na kazi za kila siku za kichungaji, parokia inaendesha pia kituo kidogo cha afya pamoja na chekechea. Kigango cha Mtunungu ni kigango cha pekee cha parokia hii.

Anuani:

Parokia ya Chikundi

SLP Ndanda

Mtwara

 
 

Parokia ya Majengo

Parokia hii ijulikanayo pia kama "Mt. Paulo Mtwara" ni parokia ya pekee ya mjini iendeshwayo na Watawa wa Ndanda. Ikiwa na takriban waumini 3000 imejitanda katika vigango vya  Likonde, Mangamba, Mtawanya, Chumvini na Naliendele. Pamoja na uchungaji wa kawaida, St. Paulo inajulikana kwa shule zake za chekechea katika vigango vyote pamoja na huduma kwa wagonjwa katika zahanati yake.

Anuani:

Parokia ya Majengo

SLP 55

Mtwara

 
 

Parokia ya Nangoo

Parokia hii ipo umbali wa kilometa 6 mashariki ya Ndanda na ilianzishwa mwaka 1981. Abate Mstaafu Siegfried alikuwa paroko wake kwa muda mrefu. Licha ya kazi za  kichungaji parokia inajishugulisha pia na huduma za shule kwa watoto wadogo na wa sekondari.

Anuani:

Parokia ya Nangoo,

SLP Ndanda

Mtwara

 
 

Parokia ya Sakharani

Parokia ya Sakharani ni moja kati ya parokia tatu ziizoanzishwa na Watawa wa Ndanda katika Jimbo la Tanga. Nyingine ni Handeni (kwa sasa chini ya mapadre wa Jimbo) na Soni. Parokia inapatikana katika maeneo ya Usambara ambako kuna mchanganyiko wa Waislamu, Wakatoliki na Waluteri. Pamoja na mchanganyiko huu mkubwa, parokia imeweza kukua na kuwa kituo muhimu si tu cha imani ila pia kwa huduma zinginezo za jamii kwa wakazi wote wa Sakharani na viunga vyake.

Anuani:

Parokia ya Sakharani

SLP 40 Soni

Tanga

 
 

Parokia ya Soni

Parokia ya Soni inapatikana nje kidogo ya mji mdogo wa Soni milimani Usambara. Pamoja na kipaumbele kinachotolewa katika shuguli za kichungaji, parokia imeweza kuwa kituo muhimu cha masuala ya afya, uendelezaji wa kilimo na mambo mengine ya kijamii.

Anuani:

Parokia ya Soni

SLP 40 Soni

Tanga

 

<<Mwanzo