Matukio Katika Historia ya Abasia

  MATUKIO MUHIMU KATIKA HISTORIA YA NDANDA
   1887:  Pd. Andreas Amrhein,  mwanzilishi wa Shirika anafungua kituo cha Misioni Emming  (kwa sasa St. Ottilien), Ujerumani.

1888: Monasteri ya kwanza kabisa katika Shirika inafunguliwa Pugu, Dar es Salaam. 1889: Pugu inaharibiwa wakati wa uasi wa Bushiri. Mabradha wawili na sista mmoja wanauawa.

1894: Prokura ya Kurasini inaanzishwa. Safari ya kupeleleza uwezekano wa kufungua misioni kusini mwa Tanganyika unafanywa. Kituo kipya kinafunguliwa Pilipili (karibu na Lindi).

1895: Kituo cha Misioni Lukuledi kinafunguliwa.

1897: Kufunguliwa kwa kituo cha misioni cha Nyangao.

 
   1905: Vituo vya Lukuledi na Nyangao vinashambuliwa wakati wa Vita vya Maji-Maji.

1906: Uamuzi wa kufungua kituo kipya cha Misioni Ndanda unafanyika. Tarehe 15.8.1906 Askofu Thomas Spreiter anaadhimisha Misa ya kwanza Ndanda.

1908: Askofu Thomas Spreiter anatabaruku Kanisa Kuu la Mt. JosephDar es Salaam.

1909: Kuanza kwa Hospitali ya Ndanda.

1917: Moja ya mapigano (battle) ya Vita vya I vya Dunia yanatokea karibu na Ndanda. Washirika wanaichukua Ndanda. Wamisionari wa Kijerumani wanatimuliwa na nafasi yao inachukuliwa na Wamisionari wa Kiswisi.

 
 

1931: Kuanzishwa kwa “Abasia Nullius” ya Ndanda.

1932: Pd. Joachim Ammann anachaguliwa kuwa  Abate wa I wa Abasia Nullius.

1933: Abate  Joachim anateuliwa kuwa askofu.

1934:  Abate-Askofu Joachim  Ammann anawekwa wakfu St. Ottilien.

1935:  Kuanzishwa kwa Ndanda Mission Press (Kiwanda cha Uchapishaji). 

 

 

 1938: Tarehe 1 Agosti Abate-Askofu Ammann anatabaruku Kanisa la Abasia Ndanda.

1942: Kutokana na vurugu za Vita vya Pili vya Dunia, Wamisionari wa Kijerumani wanalazimishwa kuondoka kutoka vituo vyao.

1945: Abate-Askofu Ammann anawasilisha ombi la kujiuzulu kwa Mwakilishi wa Kiti cha Kitume.

1946: Shamba la  Sakharani linanunuliwa.

1949: Pd. Victor Haelg anateuliwa kuwa Askofu Mwandamizi wa Ndanda. Mwezi Juni anawekwa wakfu na mwezi Disemba anachukua nafasi ya Ammann kama Abate-Askofu wa Pili wa Ndanda.

 

1972: Tarehe 18 Disemba jimbo la Mtwara linaanzishwa.

1975: Tarehe 29 Novemba Askofu Victor anafariki Ujerumani na kuzikwa katika kanisa la Abasia St. Ottilien.

1976: Tarehe 6 Februari watawa wa Ndanda wanamchagua Pd. Siegfried Hertlein kuwa Abate wa III wa Ndanda.

1991: Bradha Yohannes Mango anakuwa Mtanzania wa kwanza kufunga nadhiri za kitawa Ndanda. Mmoja baada ya mwingine wanafuata. Kwa tendo hilo, Ndanda inakuwa jumuiya ya mseto – Ndugu wa Ng’ambo na Watanzania.

 
  2001: Tarehe 14 Julai kundi la kwanza la ndugu wanne wa Kitanzania wanapokea daraja la Upadre: Pd. Placidus Mtunguja, Pd. Sylvanus Kessy, Pd. Amani Nyoni  na Pd. Philibert Mandera.

2001: Tarehe 3 November Abate Siegried anang’atuka baada ya kutumikia jumuiya     yake kwa miaka kwa robo karne.

2001: Pd. Dionys  Lindenmaier anachaguliwa kuwa Abate wa IV wa Ndanda.

2006: Mwezi Agosti Ndanda inaadhimisha miaka mia ya kuweko kwake; hii ikimaanisha pia Jubilei ya miaka mia ya Ukristu jimboni Mtwara. Ni wakati huu Jumuiya inaamua kuanzisha kituo kipya cha Kiroho pamoja na Sekondari ya Abbey.

 

 << Mwanzo