Uongozi wa Shirika

VIONGOZI WA SHIRIKA 

   

Bro.Dk.  Ansgar Stüfe OSB

Mhasibu wa Shirika 

BRADHA ANSGAR ni mtawa wa Abasia ya Münsterschwarzach kwa asili aliyefuzu kama daktari. Alizaliwa mwaka 1952 huko Bad Mergentheim katika jimbo la Stuttgart-Rottenburg. Nadhiri zake za kwanza alifunga mwaka 1980. Alitumwa Peramiho kama mmisionari na tabibu mwaka 1987. Pamoja na kuiendesha hospitali hiyo kwa miaka 17 alichaguliwa pia katika Halmashauri ya Shirika miaka ya mwanzo ya 2000. Mkutano mkuu wa Shirika wa 2004 ulimidhinisha kama Mhasibu wa Shirika - nafasi anayoishikila hadi sasa.

Abate Jeremias Schröder OSB

Rais wa Shirika 

ABATE JEREMIAS alizaliwa mwezi Disemba 1964 katika mji mdogo wa Bad Wörishofen jimboni Augsburg. Alifunga nadhri za kwanza mwaka 1985 St. Ottilien. Mwaka 1992 alipewa daraja la upadre. Baada ya mtangulizi wake Notker Wolf kuchaguliwa kuwa Abate Primate mwaka 2000, jumuiya ya St. Ottilien ilimchagua  kuwa abate wake mkuu wa 6. Tangu 2000 hadi 2012 alishikilia kofia mbili: Abate Mkuu wa St. Ottilien na Rais wa Shirika. Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2008 yalitenganisha kofia hizo mbili. Hivyo mwaka 2012 alipochaguliwa kuwa Rais wa Shirika, alijiuzulu kama Abate Mkuu wa St. Ottilien.

Pd. Maurus Runge OSB

Katibu wa muda  Shirika

PADRE MAURUS RUNGE anatoka katika jumuiya ya KÖNIGSMÜNSTER, Ujerumani. Mwaka 2016 Pd. Romain Botta (sasa Abate wa Agbang) alimpisha Pd. Pambo Mkorwe katika nafasi ya ukatibu. Pd. Pambo aliweza kushikilia nafasi hiyo kwa miezi michache tu, kwani hapo Julai 2017 jumuiya ya Mvimwa iliweza kumchagua kama abate wake wa tatu. Kwa sasabu hiyo Pd Maurus anakaimu nafasi hiyo. Tunategemea kumpata katibu mpya Januari 2018.

  Halmashauri ya Shirika  

Licha ya maofisa waliotajwa hapo juu ambao kazi yao ni kuratibu na kuendesha kazi za kila siku za Shirika, uongozi wa Shirika unakamilishwa na timu ijulikanayo kama "Halmashauri ya Shirika" ambayo ina wajumbe kutoka nchi mbalimbali. Mkutano Mkuu wa Shirika (2016), uliwachagua wafuatao kama wajumbe wa Halmashauri kwa kipindi cha miaka 4 ijayo:

Abate Michael Reepen  (Ujerumani), Pd. Noach Heckel  (Ujerumani), Pd. Christian Temu (Tanzania), Priori John Baptist (Kenya), Abate Blasio Park (Korea Kusini),  Pd Javier Suarez (Hispania) na Abate Romain Botta (Togo). Rais, Mhasibu na Katibu wa Shirika  wanaingia katika Halmashauri kutokana na nyadhifa zao (ex officio). 

<<Mwanzoni