Chuo Cha Uuguzi

CHUO CHA UUGUZI NDANDA

   Historia: Shule ilianzishwa mwaka 1930 na Sr. Dr. Theckla Stinnesbeck OSB na ilifungwa mwaka 1939 wakati wa vita vya pili vya dunia. Baada ya vita mwaka 1945, kozi fupi ya miezi 18 kwaajili ya wakunga vijijini ilianza na mwaka 1950 Wizara ya Afya ya Kikoloni ilitoa ruhusa kuanzisha mafunzo ya miaka 2 kwaajili ya wakunga. Mafunzo ya Uuguzi yalianza mwaka 1965 ambayo yalikuwa ni kozi ya miaka 3 na Wahitimu walisajiliwa kama wauguzi Daraja la B.  
  Diploma: Kotoka mwazo tangu shule ilipoanzishwa ilikuwa inatoa mafunzo kwa jinsia zote (kike na kiume). Mnamo mwaka 1970, kozi ya miaka miwili kwa ajili ya Ukunga ilisimamishwa. Mwaka 1983 kozi ya mwaka mmoja ya uuguzi awali ilianzishwa na kozi hiyo ilisimamishwa tena mwaka 1993. Mwaka 1994 mwezi Septemba, kozi ya miaka 4 ya Diploma ya Uuguzi ilianza.  
  Dira: Kuwaandaa wauguzi wataalamu na wenye uwezo kutoa huduma bora kwa wagonjwa, na wenye heshima kwa uhai tangu mimba inapotungwa mpaka kifo kinapotokea.

Utume: Kutoa elimu inanayoweza kufikiwa na wanafunzi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya huduma za uuguzi. Hii itafikiwa kwa kuandaa mipango ya ubunifu inayoonyesha mahitaji na hali ya sasa ya jamii.

 
 

Maadili ya Msingi: • Kueshimu, kutunza na kuendeleza uhai tangu mimba inapotungwa mpaka kifo • Kuwahudumia wagonjwa kwa usawa bila kujali rangi, elimu, kabila, dini, jinsia, hadhi ya mtu kijamii, kiuchumi na kimwili • Kuzingatia maadili ya Kikristu na kanuni za maadili ya Kanisa Katoliki • Kushirikiana na wadau wengine katika kazi.

Masharti ya Usahili: Mafunzo yapo wazi kwa mwombaji ambaye angalau amemaliza elimu ya kawaida ya Sekondari ya kidato nne kwa Tanzania (CSEE) na kufahulu katika masomo ya sayansi; Bailogia, Kemia, fizikia/hesabu kwa kupata angalau daraja D au zaidi. Mwombezi awe na uwezo mzuri na wa kutosha katika lugha ya Kiigereza.

 
 

 

Watumishi: Kuna walimu 7 wa muda wote kwaajili ya uuguzi kiujumla, Afya ya Akili na Ukunga pamoja na Mkufunzi 1 wa Kliniki. Wapo pia watumishi wasaidizi 19.

 

 

Anuani:

Ndanda School of Nursing

SLP Ndanda - Via Mtwara

<< Mwanzoni