Idara ya Ujenzi

IDARA YA UJENZI ya Abasia imekuwa kati ya idara muhimu kabisa katika historia ya Ndanda kama kituo cha Kimisionari. Imepanga na kusimimia miradi mbalimbali ya ujenzi  kama:

          - Ujenzi wa Makanisa, Shule na Hospitali

          - Ujenzi wa nyumba za maparokia na zile za Kitawa,

          - Ujenzi wa madaraja,

          - Ujenzi wa majengo mapya na ukarabati wa yale yanayochakaa.

  Katika picha ya juu kushoto, kiongozi wa idara hiyo Bradha Andreas Kurzendorfer anaonekana akielezea mpango wa ujenzi wa Kituo cha Kiroho cha Zakeo kwa wageni. Kituo hicho ambacho kilijengwa kwa muda wa miaka 4 hivi kina uwezo wa kupokea wageni zaidi ya hamsini kwa mara moja. Baadhi ya Majengo yake yanaonekana katika picha hapa kushoto.  
  Miradi mingine mikubwa mipya iliyotekelezwa na Idara hii ni ujenzi wa bawa jipya la monasteri ya Ndanda, ujenzi wa bwalo katika Sekondari yetu, ujenzi wa chumba cha upasuaji cha hospitali na majengo mapya ya chuo cha Uuguzi Ndanda. Picha mbili kushoto na chini kushoto  zinaoneshea bawa jipya la monasteri.  
 

Licha ya shughuli za kusanifu,  kujenga na kukarabati majengo, Idara hii inajishughulisha pia na usanii wa uchongaji wa mawe. Meza za Altare, visima vya ubatizo, mimbari, sanamu mbalimbali na viti vya altareni (viti vya enzi vya Maaskofu pia) vimekuwa vinatengenezwa na idara hii na kuuzwa katika majimbo mengi nchini. 

     Picha kulia kutoka juu: 1. Mafundi baada ya kumaliza kuchonga sanamu ya Mt. Benedikto, 2. Umaliziaji wa kiti cha kiaskofu na mimbari, 3. Umaliziaji wa  meza ya altare. 4. Picha ya hapa kulia inaonesha altare katika kanisa la abasia iliyotengenezwa na idara hiyo.

 

<<Mwanzoni