Utunzaji Mazingira

 

 

MBAO NI MALI GHAFI katika kiwanda chochote cha samani. Mali ghafi hii itapatikana tu iwapo misitu ya asili itatunzwa na miti mipya kupandwa.  Idara yetu ya Useremala iko makini katika jambo hili kama picha hizi zinavyoonesha.

Miche michanga hupandikizwa. Umwagiliaji wa mara kwa mara ni wa lazima. Miche ya Mitiki kitaluni.
     
Miche hii iko tayari kuoteshwa. Mitiki hukua kwa kasi ikitunzwa vizuri.  Kutokana na kukua kasi kwa magugu ...
     
... misitu yetu hupaliliwa kwa matrekta maalum ....  ... ili kuhakikisha miti inakua bila kukabwa na magugu.  Miti hii huitaji kufyekewa mara chache kwa mwaka.

Baada ya kazi ya miaka michache, matunda huanza kuonekana.

Abasia ilipata tuzo  la kitaifa Dodoma, 2010 kwa kutunza mazingira.

Msitu uliokomaa unasaidia kuleta uwiano katika hali ya hewa.

<< Mwanzoni