Ushonaji na Mitindo

Idara ya Ushonaji Ndanda chini ya Bradha Romainus Nnunduma ni kati ya idara mpya katika abasia. Kwa miaka mingi huduma za nguo kwa watawa ilikuwa inatolewa au na mafundi wa nje (kwa nguo za kiraia) au na Masista jirani zetu (kwa mavazi ya kitawa). Baadaye jumuiya iliamua kuwa na fundi wake mwenyewe awezaye si tu kutosheleza mahitaji ya jumuiya bali pia mwenye uwezo na umahiri wa kufundisha wengine na pia kutoa huduma bora ya ushonaji kwa wale wanaohitaji huduma hiyo. Ndugu yetu (akiwa mitamboni kulia) emejidhihirisha kuweza yote mawili: kushona mavazi ya kitawa na pia kutoa huduma hiyo kwa wengine wahitajio ufundi wake.         
Kwa kusaidiana na mafundi kadhaa waliobobea katika ubunifu wa mitindo mbalimbali ya ushonaji wa nguo za akina mama, wanaume, nguo za shule na za watoto kwa ujumla, Bradha Romanus anajivunia kutoa huduma bora na ya uhakika kwa walae wote wanahitaji huduma hiyo. Picha hii ya kulia inamwonesha (kushoto) akiwa na mafundi wake wasaidizi katika chumba cha ushonaji.  

Pamoja na nguo za "kiraia," idara ya ushonaji inajishughulisha sana na ushonaji wa mavazi ya kitawa na yale ya liturjia kwa ujumla. Katika picha hizi mafundi wanaonekana wakikata vitambaa vyeupe katika matayarisho ya kushona kanzu za watawa. Lakini kama tulivyosema hapo juu, idara hii inajishugulisha na mitindo ya aina zote za nguo na kwa makundi yote katika jamii.

 

<<Mwanzoni