Magari & Chuma

KWA MIAKA MINGI  karakana ya kukarabati magari ya Ndanda imekuwa inatoa mchango mkubwa katika utengenezaji wa magari  kwa ajili ya wamisionari, majimbo ya jirani na kwa watu binafsi. Siku hizi "Gereji Ndanda" kama inavyojulikana, inajivunia kuwa na mafundi wazoefu wawezao pia kutoa elimu ya nadharia na ya vitendo kwa vijana wanajiunga na fani hiyo.

Picha: Mafundi na wanafunzi wakipeana maelekezo (kushoto) huku fundi mmojawapo akikarabati 'cylinder block' ya gari (kulia).

  Kazi bila vitendea kazi haiendi. Gereji Ndanda inaweza kutoa huduma nzuri kwa wateja na wanafunzi kutokana na kuwa na vifaa vizuri vya kutendea kazi. Kushoto mwanafunzi akiwa na mashine ya ulainishaji wa vyuma huku mafundi wengine wakiendelea na ukarabati wa maghari ya wateja (kulia).  
 

Idara ya Ufundi Chuma imekuwa pia kati ya idara muhimu kabisa za karakana zetu na imekuwa inafanya kazi kwa karibu sana na gereji yetu pamoaja na idara ya ujenzi. Kazi zake muhimu:-

- Uchongaji, ukataji na uchomeaji wa vyuma vya aina zote (kulia),

- Usanifu na uundaji wa gatasi kwa ajili ya majengo (kushoto).

- Uundaji na utengenezaji wa milango, madirisha na mageti ya chuma,

- Ukarabati wa mashine za aina mbalimbali.

 
  Mafundi wetu pamoja na wanafunzi wao kwa kutumuia vifaa vilivyopo na ubunifu wao wanaweza kutengezeza vifaa mbalimbali. Mfano wa vifaa hivyo ni mapipa maalum ya alumini yatumikayo kuhifadhia nafaka kama picha ya kulia inavyoonesha.  

 <<Rudi Mwanzoni