Ufundi & Kompyuta

KUTOKANA NA SHUGHULI mbalimbali zinazoendeshwa na Watawa,  Ndanda imekuwa si tu kituo cha kiroho, ila pia kituo cha mafunzo mbalimbali. Licha ya elimu ya sekondari na ile ya uuguzi, vijana wanaotaka kupata mafunzo ya ufundi wanaweza kufikia azima yao hiyo kwa kujiunga na "Ufundi Ndanda." Katika chuo hiki vijana hupata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali kama: Ufundi Chuma, Ufundi Magari, Useremala, Ujenzi, Ufundi Bomba, Mambo ya Uchapishaji, Ufundi Viatu, Ushonaji, Ufundi Umeme, Kompyuta/Uhazili, n.k.

 

Picha kushoto na kulia: Wanafunzi wa Uhazili/Komputa wakiwa darasani.

 

Kutokana na kuwepo kwa karakana zenye vifaa vya kutosha na waalimu/mafundi wenye uzoefu wa miaka mingi, Wanafunzi wetu wa ufundi wanayo nafasi nzuri ya kujifunza kwa vitendo katika karakana hizo.

Kushoto: kitengo cha ufundi magari;

                                                         Kulia: sehemu ya mazoezi ya ufundi chuma. 

 
 

Vijana wafikao kwetu kwa lengo la kujifunza useremala wanayo nafasi kubwa ya kuwa mafundi wazuri na hodari wawezao kujitegemeza kwa siku za mbele. Msisitizo mkubwa unatiliwa katika kujifunza kwa vitendo kama picha kushoto inavyoonesha. Matokeo yake ni samani zenye ubora wa juu (tazama picha kulia). 

 
 

 Kiwanda chetu cha uchapishaji wa vitabu cha Ndanda Mission Press hupokea wanafunzi kadhaa kila mwaka. Wanafunzi hao hujifunza mambo mbalimbali kuanzia "book-binding," jinsi mashini za kuchapa zifanyavyo kazi na uchapishaji wenyewe.Picha ya kulia na kutosho zaonesha wanafunzi na mafundi wakiwa kazini ndani ya majengo ya kiwanda.

 
 

 

Wanafunzi wetu hawajifunzi kitu kimoja. Picha ya kushoto, kwa mfano, inaonesha mafundi na wanafunzi wa kitengo cha magari wakifunga mtambo wetu wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji (turbine). Elimu itolewayo ni zaidi ya kuziba pancha au  kutoa grisi katika 'gear box.' ...

Kushoto mafundi na mwananfunzi wa idara ya chuma wakitengeneza gatasi.


<<Mwanzoni